WASIFU WETU


DIGNITY Kwanza

DIGNITY Kwanza-Community Solutions, ni shirika lisilo la kiserikali ambalo limesajiliwa hapa Tanzania chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2005. DIGNITY Kwanza imeanzishwa na kikundi cha watu binafsi ambao walikuwa wanafanya kazi katika shirika la Asylum Access Tanzania (AATZ) ambalo lilikuwa linafanya kazi Tanzania na kusitisha shughuli zake mwezi Juni mwaka 2018.

DIGNITY Kwanza imeanzishwa ili kuweza kuendeleza huduma ambazo zilikuwa zikifanywa na AATZ kama, huduma ya kisheria, kuinua jamii kwenye maswala ya kiuchumi na maisha katika jamii. DIGNITY Kwanza haitaendelea kuhudumia wakimbizi tu bali itahudumia pia jamii ya makundi yaliyo katika mazingira hatarishi na wasiojiweza.

Maono yetu tunaiona Tanzania ni sehemu ambayo mtu anaishi kwa utu na uhakika wa kupata fursa ambayo itamuwezesha kujikimu na kuchangia maendeleo katika kujenga taifa.

Dhamira yetu ni kulinda na kukuza utu wa binadamu kwa makundi yaliyotengwa na yanayoishi katika mazingira magumu kuwapa maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia elimu, misaada na kuwawezesha.


NINI KILICHOPO KWENYE JINA? .

Utu wa ubinadamu na maendeleo ni pande mbili za sarafu moja. Wakati kila mtu katika jamii anaweza kuishi kwa kuheshimiwa utu wake, maendeleo yake kijamii na kiuchumi ni muhimu yazingatiwe.

Kwa bahati mbaya imekuwa mwenendo haswa katika nchi zinazoendelea, kutibu dhana hizi mbili kama za kipekee. Mpango wa maendeleo na miradi haijatengenezwa kuunda hali inayoheshimu, kulinda na kuthibitisha utu wa binadamu, wakati haki za binadamu, ambayo ni sehemu muhimu ya heshima ya binadamu inachukuliwa kama kikwazo kwa maendeleo. Kwasababu hiyo, kikundi fulani cha watu hukataliwa na kuathirika, na wanakabiliwa na shida kama vile kukiukwa kwa haki zao za msingi, umaskini uliokithiri, kutengwa, ufikiaji mdogo wa huduma za kijamii, ukosefu wa ajira na upungufu wa fursa za kujikimu na kuchangia vya kutosha katika ujenzi wa taifa.

DIGNITY Kwanza tunaamini kwamba haki za watu zikilindwa, kila kitu kitajiweka mahala pake, hiyo ndiyo ‘’DIGNITY Kwanza’’.

HUDUMA TUNAZOTOA .

1. Msaada wa kisheria kwa mtu mmoja mmoja na makundi (ushauri wa kisheria, elimu na uwakilishi)

2. Uwezeshaji wa jamii na msaada

3. Maendeleo na misaada ya kibinadamu.

4. Utetezi, kukuza uelewa na ushawishi

WALENGWA .

1. Wakimbizi, waombahifadhi, wahamiaji walio katika mazingira hatarishi.

2. Watu wasio na utaifa na watu walio katika hatari ya kukosa utaifa.

3. Watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri (na uangalizi maalum kwa wanawake, watoto na vijana)

Our social pages updates

Tanzania useful links

Useful Websites

Constitutionals

Refugees Agency

MAENEO YETU MAKUU YA KIMKAKATI


Top